Jaden Smith Atoa Mchango Huu Kwa Wasiojiweza

Jaden Smith Atoa Mchango Huu Kwa Wasiojiweza

Mwigizaji na msanii maarufu kutoka Marekani, Jaden Smith, ameendelea kuonyesha dhamira yake ya kusaidia jamii ambapo ameripotiwa kufungua mgahawa kwa ajili ya kutoa chakula bure kwa watu wasiojiweza.

Mgahawa huo, unaojulikana kwa jina la ‘I Love You Restaurant’, umefunguliwa rasmi mjini Los Angeles, ikiwa ni mwendelezo wa kampeni aliyoanzisha mwaka 2019 kupitia gari la chakula cha msaada.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mgahawa huo, Jaden alisisitiza kuwa kila mtu anastahili kula chakula kizuri.

“Watu walioko mitaani hawahitaji huruma pekee wanahitaji heshima. Kupitia mgahawa huu, nataka kuwapa chakula kizuri katika mazingira ya heshima na upendo. Iwapo huwezi kulipa, bado unakaribishwa kula. Ikiwa unaweza kulipa, unalipia pia chakula cha mtu mwingine. Huo ndiyo moyo wa mgahawa huu,”amesema Jaden

Ikumbukwe wazo la ‘I Love You Restaurant’ lilianza kwa kutoa chakula kwa watu walioko mitaani kupitia food truck hata hivyo kutokana na uhitaji mkubwa na mwitikio kwa jamii Jaden aliamua kubadilisha huduma hiyo kuwa mgahawa wa kudumu unaofunguliwa kila siku huku akishirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali.

Hata hivyo Jaden Smith, ambaye pia ni mtoto wa nyota wa filamu Will Smith, amesema kuwa ndoto yake ni kupanua huduma hizo katika miji mingine mikubwa duniani.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags