Kesi Ya Asap Rocky Kuendelea 2026

Kesi Ya Asap Rocky Kuendelea 2026

Ikiwa imepita takribani wiki moja baada ya rapa Asap Rocky kuachiwa huru kufuatia na mashtaka ya shambulio la jinai lililofunguliwa na A$AP Relli (Terell Ephron), sasa inaelezwa kuwa kesi hiyo inarudi tena mahakamani mwaka ujao.

Licha ya Rocky kutokuwa na makosa yoyote lakini Relli anaendelea na kesi hiyo ya madai akilenga kumwajibisha rapa huyo katika mahakama ya kiraia nchini Marekani.

Jana Jumatano Februari 26, Jaji wa Mahakama Kuu ya Kaunti ya Los Angeles, William Fahey, alithibitisha rasmi tarehe ya kusikilizwa kwa kesi hiyo kwa mara nyingine ambayo itakuwa Januari 12, 2026.

Aidha kwa mujibu wa Wakili wa Relli, Melisa Mikail, apokuwa kwenye kikao cha mahakama cha kufungua kesi hiyo amefunguka kuwa mteja wake hatarudi nyuma katika kesi hiyo.

“Tuna dhamira ya kuendelea na kesi hii. Kiwango cha uthibitisho katika kesi ya jinai ni cha juu zaidi kuliko kiwango cha uthibitisho kinachohitajika katika kesi ya madai. Bado tunaamini kuwa madai yetu yana nguvu, na tunakusudia kuyasikiliza kikamilifu mahakamani,” amesema Melisa

Utakumbuka kuwa Rocky alifunguliwa mashitaka na aliyekuwa rafiki yake A$AP Relli aliyemtuhumu kwa kumshambulia kwa kutumia bunduki tukio lililotokea 2021.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags