Konde Boy Awapiga Mkwara Wasanii Wa Uganda

Konde Boy Awapiga Mkwara Wasanii Wa Uganda

Baada ya kutokea sintofahamu katika tamasha la Furaha City Festival lililofanyika Desemba 7, 2024 nchini Kenya. Mwanamuziki Harmonize ametoa onyo kwa wasanii wa Uganda.

Konde ambaye anatarajia kwenda kutumbuiza katika nchi hiyo Desemba 28, 2024, katika tamasha la Arua City amewataka mashabiki kuwatuliza wasanii wao wakorofi maana hatakuwa na msamaha na mtu.

“Uganda team no excuses coming kama kuna msanii wenu mkorofi mkorofi mwambieni kabisa atapigwa nakamata natia vibao, show itafanyika then tutakutana police hakuna wa kunizuia kuimba labda mwenyewe president Kagame,” ameandika Konde Boy katika ukurasa wake wa Instangram

Hata hivyo licha ya kutokea sintofahamu kwenye tamasha lililofanyika jijini Nairobi, jana Desemba 10, 2024 Diamond alitoa maelezo kuhusiana na kilichotokea huku akidai vurugu ndio sababu ya kuondoka bila kutumbuiza.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags