Mwanamuziki kutoka Marekani Taylor Swift ameitunuku timu yake ya ‘Eras Tour’ bonasi ya dola 197 milioni kama ishara ya kuthamini juhudi zao katika ziara yake hiyo.
Kwa mujibu wa tovuti mbalimbali zinaeleza kuwa msanii huyo ametoa maokoto hayo katika timu yake nzima ikianziwa na madereva wa maroli, watu wa densi, wabunifu wa mavazi yake mpaka waandishi waliokuwa wakiripoti kuhusiana na ziara yake.
Ziara ya ‘Eras Tour’ inatarajia kutamatika katika uwanja wa BC Place Vancouver Desemba 8, 2024 huku mashabiki zaidi ya milioni 10 wakinunua tiketi kwa ajili ya show hiyo ambayo inataajia kukusanya zaidi ya dola bilioni 2 katika mauzo ya tiketi.
Aidha endapo ziara hiyo itafanikiwa kukusanya mapato hayo katika tiketi itaweka rekodi mpya kama ziara ya muziki iliyoingiza mapato makubwa zaidi katika historia.
Leave a Reply