Miongoni mwa albamu za muziki wa Bongo Fleva zilitoka 2024 ni pamoja na The God Son ya kwake Marioo na Therapist ya Jay Melody. Albamu zote hizo zimefanikiwa kufanya vizuri kwenye mitandao ya kijamii na majukwaa ya kuuzia muziki, lakini hazina wasanii wa Hip-hop walioshirikishwa.
Albamu ya Jay Melody ambayo ilitoka Aprili 25, 2024 ikiwa na jumla ya track 14, hakuna msanii yeyote wa Hip-hop aliyeshirikishwa na hivyo ndivyo ilivyo pia kwa Marioo aliyetoa The God Son, Novemba 29, 2024 ikiwa na jumla ya track 17.
Kwa mujibu wa rapa Conboi ambaye ni Hitmaker wa 'Till I Die' amewashauri wasanii wa Bongo Fleva kushirikisha wana-hiphop kwenye albamu zao zijazo.
"Nadhani wao wenyewe wanaweza kuwa na sababu za msingi kwanini hawajafanya kazi na rappers lakini kazi zao wote ni kali na nimezipenda, kwa ushauri wangu kwenye kazi zao zinazokuja washirikiane na rappers," amesema Cannabino alipokuwa akifanya mahojiano Clouds Media.
Hata hivyo Marioo na Jay Melody wamekuwa na muunganiko mzuri wanapokutana na wasanii Hip-hop kama ambavyo ilitokea kwenye Loyarty ya Darassa ft Marioo na Nandy, Pisi ya Malume Ft Marioo, Mapozi ya Diamond Platnumz Ft Mr Blue na Jay Melody.
Leave a Reply