Baada ya kutangaza uhusiano wake mpya na mpenzi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Edo, Natasha Osawaru, sasa msanii huyo amemvisha pete mpenzi wake huyo.
Kufuatia na video zinazoendelea kusambaa katika mitandao ya kijamii msanii huyo alionekana akiwa nyumbani kwake na Natasha huku kukiwa na tukio muhimu ambapo alimvisha pete ya uchumba mbunge huyo.
Mapema wiki hii 2Face alichapisha picha ya Mbunge huyo akiambatanisha na ujumbe wa kudai kuwa ndio mwanamke atakayefunga naye ndoa tena.
Utakumbuka msanii huyo aliyewahi kutamba na ngoma ya ‘African Queen’ alizua gumzo katika mitandao ya kijamii mwishoni mwa Januari 2025 baada ya kutangaza kutengana na aliyekuwa mke wake baada ya kudumu naye kwa miaka 13 huku akidai kuwa kwa sasa wapo katika taratibu za kupeana talaka.

Leave a Reply