2face Atambulisha Africa Queen Mwingine

2face Atambulisha Africa Queen Mwingine


Baada ya mwanamuziki kutoka Nigeria Innocent Idibia '2Face' kutangaza kuachana na mkewe Annie Idibia, baada ya kudumu kwenye ndoa kwa miaka 13, hatimaye ametangaza kuwa na uhusiano na Mbunge wa Jimbo la Edo, Natasha Osawaru.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram jana Jumanne Februari 11, 2025 alichapisha picha ya Mbunge huyo akiambatanisha na ujumbe wa kudai kuwa ndio mwanamke atakayefunga naye ndoa tena.

“Natasha ni mwanamke mchanga, mwelevu, na wa ajabu. Nampenda, anapendeza, na nataka kumuoa,” amesema 2Face huku akisisitiza kuwa Mbunge huyo asihusishwe na talaka yake na badala yake lawama zote ziende kwake.

Msanii huyo aliyewahi kutamba na ngoma ya ‘African Queen’ mwishoni mwa Januari 2025 alitangaza kutengana na aliyekuwa mke wake baada ya kudumu naye kwa miaka 13 huku akidai kuwa kwa sasa wapo katika taratibu za kupeana talaka.

Aidha kutokana na watu kuwa na maoni tofauti mwanamuziki huyo aliamua kufuta chapisho hilo huku akiwaacha mashabiki na wadau wake njia panda kama ni kweli alichokizungumza au ni kiki.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags