50 Cent amcheka Rick Ross baada ya kushambuliwa Canada

50 Cent amcheka Rick Ross baada ya kushambuliwa Canada

Mkali wa Hip-hop Marekani 50 Cent, aonekana kufurahishwa na video inayosambaa mitandaoni ikimuonesha ‘rapa’ Rick Ross akishambuliwa nchini Canada.

Kupitia ukurasa wa X (zamani twitter) 50 Cent ali-share video akizungumzia suala la Rick na kueleza kuwa tukio hilo lilikuwa lakusikitisha sana huku mwishoni akiangua kicheko cha kumdhihaki msanii huyo.

“Ninatumai kwamba kaka huyo alifika nyumbani salama. Na natumai kuwa sasa ana mtazamo tofauti na hisia bora zaidi ya nini cha kufanya na kisichopaswa kufanya ukiwa nchi za watu” amesema 50

Wikiendi hii Rick Ross na washikaji zake walishambuliwa na mashabiki pamoja na watu wa Drake jijini Vancouver, Canada baada ya kupiga wimbo wa Kendrick Lamar ‘Not Like Us; alipomaliza kufanya show yake.

Rick Ross ‘Rozay’ alikwenda nchini humo kwa ajili ya kufanya show katika tamasha la ‘Ignite Music Festival’ ambapo baada ya kutumbuiza ngoma zake zote ndipo akacheza ngoma hiyo ya Lamar ambayo aliitoa kwa ajili ya kumchana Drake.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags