Aina za biashara unazoweza kuzifanya kwa mtaji mdogo

Aina za biashara unazoweza kuzifanya kwa mtaji mdogo

Hellow! Watu wangu wa nguvu, bwana bwana kama kawaida yetu na kauli mbiu yetu inavyosema kuwa hakuna kukaa kizembe hadi biashara ikushinde udugu, sasa leo nimekusogezea mada ambayo itakujuza baadhi ya biashara utakazo zifanya ukiwa na mtaji mdogo.

Acha kulialia umasikini, hizi hapa aina za biashara unaweza kuzifanya kwa mtaji wa kuanzia elfu 10 hadi 50, udugu kuwa beki tatu unataka mwenyewe, ungana nami kujifunza mwanzo mwisho.

  • KUUZA DAGAA WA BUKOBA

Dagaa hawa wanapatikana masoko mengi, hawa wanakua hawana mchanga kabisa, wanauzwa kg moja elfu nane, huwa inashuka hadi elfu tano, hawa unanunua vifuko unapack unauza mtaani kifuko buku. 

Kwenye kilo moja unaweza toa vifuko 15 sawa na elfu kumi na tano so elfu mbili vifuko elfu tano faida. Pia unaweza uza dagaa wa Kigoma, Zanzibar au Mwanza waliokaangwa.
 

  • BIASHARA YA MATUNDA

Siku hizi watu wengi haswa maofisini wanapenda kula matunda wakati wa asubuhi na mchana, cha kufanya, andaa kwa usafi matunda yako hapa, unaweza tumia elfu kumi na tano tu.

Unanunua matunda mchanganyiko tikiti, ndizi, tango, karoti, papai, parachichi matunda ya elfu kumi na tano buguruni au katika soko lolote linalouza matunda then nunua vifungashio vile vya kuwekea matunda, pack matunda yako ambapo yakiuzika vyema unaondoka na faida nusu kwa nusu. Kwa ile packet unauza 1500 au 2000.

 

  • JUICE ZA MATUNDA

Matunda ya elfu kumi waweza toa hadi lita kumi za juice ambapo lita moja ni sawa na glass tano au nne za juice, so kwenye lita kumi upata glass 40 sawa na elfu ishirini ukitoa matunda, sukari na viglass, una faida elfu tano. kwa kawaida glass ya juice mjini ni shilingi elfu 2 hadi elfu 3 so ni wewe kuchangamkia fursa na tena ukiwa umepata ofisi ya kupeleka kila siku aaaah! Wewe ni tajiri hapa mjini.

 

  • BIASHARA YA BITES

Hapa nazungumzia crips, sambusa, chapati, maandazi, mihogo ya kukaanga, vitumbua, karanga za mayai, ubuyu, korosho, visheti etc unaweza sambaza vitafunwa maofisini as package kwamba pack moja ina andazi, sambusa, chapati na kachori au ukauzia nyumbani, moja ya vitafunwa hivyo. Bites pia unaweza peleka kwenye maduka na supermarket, faida yake huwa nusu kwa nusu ya mtaji unaoutoa.

 

  • BIASHARA YA VINYWAJI BARIDI STENDI ZA DALADALA

Unaweza uza hata kwenye ndoo kama huna deli. Watu wanasema mwanzo mgumu, naamini ukitilia maanani biashara yako, one day utakuwa na deli lako special. Cha kufanya, nunua mabarafu, nunua vinywaji, tafuta kijana au wewe mwenyewe uza stend za daladala, inalipa saaana zaidi ya sana.

 

  • BIASHARA YA UJI WA ULEZI, UJI WA MCHELE NA MAKANDE

Kodi toroli, jaza chupa zako za uji aina zote, tembeza kwenye magereji na sehemu za bodaboda, unaweza tembeza mwenyewe au ukampa kijana faida ni mara mbili ya mtaji ukitumia elfu kumi, jua utapata elfu 30. Kuna baadhi ya watu wanaidharau sana hii biashara lakini ina faida sana, jaribu ujionee maajabu.

 

  • BIASHARA YA MBOGAMBOGA

 Kuna baadhi ya watu wanawadharau wale wamama wanaotembeza katika mitaa yao ila wanapata faida kuliko hata mnavyofikiria. Ukishatoka kununua mboga zako maana mafungu unayouziwa sokoni ni makubwa so unazigawanisha mara mbili na unaanza kutembeza kwa majirani na marafiki, kama umetingwa unampa kijana ukauza mtandaoni unaoeleka kwa order ukatembea kwenye mahotel na migahawa kuomba uwauzie mboga mboga na utakapo anza kuzoea biashara hiyo basi unatafuta sehemu na kuanza kuotesha mboga zako. 

Cha kukuongezea kikubwa, watu wote wenye mafanikio waliweka aibu kando. Wengi hukata tamaa kufanya biashara, watapata wapi wateja jamani, saivi dunia ni kama Kijiji, mimi nipo Dar but watu wa Songea wanakula karanga zangu, natuma bidhaa Arusha, smartphone yako ndio duka lako namba moja, phonebook yako ndio wateja wako. Achana na magroup ya umbeya WhatsApp, hakikisha unazungukwa na watu ambao mtafanyabiashara, utatangaza ubuyu watanunua majirani, kuzurula kila mtaa beba vipakti vya ubuyu, uza karanga etc.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags