Akon: Wanaume Wanatakiwa Kuwa Na Wanawake Wengi

Akon: Wanaume Wanatakiwa Kuwa Na Wanawake Wengi


Mwigizaji na mwanamuziki Akon Thiam akiwa katika mahojiano na The Joe Budden Podcast ametoa maoni kuhusu mahusiano kwa kusema wanaume wanatakiwa kuwa na wanawake wengi.

“Wanawake barani Afrika wanakutendea kama mfalme. Hawashindani na wewe, hawapiganii usawa kwa sababu wanaelewa kwamba wanaume na wanawake hawawezi kuwa sawa.

Kila mtu ana jukumu lake, hilo ndilo msingi wa maisha, na kama mwanamke haelewi nafasi yake maishani, kila mtu anachanganyikiwa. Hapa Marekani, hata ukitamka neno ‘jukumu’ kwa mwanamke, wanakasirika,” amesema Akon

Mbali na hilo Akon amefunga kuwa ni asili ya wanaume kuwa na wanawake au wenza wengi na katika tamaduni nyingi za Kiafrika, inachukuliwa kama jambo la kawaida na linapaswa kueleweka kama sehemu ya asili ya mwanaume, hivyo wanawake wanatakiwa kuelewa hilo.

Utakumbuka Akon ana watoto wa tano kwenye ndoa yake na Tomeka Thiam na wengine wanne akiwapata kutoka kwa wanawake tofauti tofauti hadi sasa nyota huyo ana watoto 12.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags