Alikiba awajibu wanaodai yeye ni jeuri

Alikiba awajibu wanaodai yeye ni jeuri

Mwanamuziki anayetamba na EP aliyoipa jina la ‘Starter’, Alikiba amewajibu baadhi ya watu wanaodai kuwa msanii huyo ni jeuri.

Alikiba amefunguka kupitia mahojiano yake aliyoyafanya na media yake ya Crown Fm ambapo ameweka wazi kuwa yeye sio mjeuri ni vile tuu hawezi kumsujudia binadamu mwenzake.

"Siwezi kumsujudia binadamu mwenzangu na hata kama ukihitaji nikusujudie basi sijui jinsi gani ya kufanya mimi ni mtu ambaye ukinikwaza nakufata moja kwa moja kukwambia kama umenikosea sasa mara nyingi nikifanya hivyo naonekanaga mjeuri huyo ndiyo mimi na siwezi kuigiza maisha. "Alisema Alikiba

Mbali na hayo wakati wa mahojiano yake hayo pia alifunguka kuhusiana na kitu ambacho anakijutia kwa wakati wote wa maisha yake kwenye muziki ambapo ameeleza kuwa ni kusimama kufanya muziki kwa muda wa miaka mitatu.

Utakumbuka kuwa mwaka 2012 Alikiba alisimama kufanya muziki kwa miaka mitatu huku akitaja sababu ya kufanya hivyo ni kutuliza kichwa chake na kuwekeza katika biashara na kusimamia malezi ya mtoto wake, kwa mujibu wa tovuti ya Mwananchi.

Kwa sasa Alikiba anatamba na Ep yake ambayo imetoka mapema siku ya jana Septemba 20, 2024 ikiwa na nyimbo saba ambazo ni Nahodha Acoustic, Chibaba, Bailando, Kheri, Top Notch, Hatari na Nahodha.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags