Mustard ni miongoni mwa watayarishaji wa muziki wa Hip-hop wanaofanya vizuri duniani. Akifanikiwa kutengeneza ngoma kali za wasanii wakubwa ikiwa ni pamoja na 'Ballin' alioshirikiana na Roddy Ricch. Lakini kubwa kuliko ni ule mkwaju wa Kendrick anaotumia kumchapia Drake 'Not Like Us'.
Mafanikio ya wimbo huo ambao umejinyakulia umaarufu makubwa na kuteka hisia za wapenzi wengi wa muziki, umeweka historia kwake kwa kuwa kati ya kazi zake zinazofanya vizuri duniani huku ukiwa umewarusha wengi kwenye mashindano ya Super Bowl 2025 baada ya kumpandisha jukwaani nyota wa mpira wa tennis, Serena Williams.
Kufanya kazi na Kendrick Lamar kwenye wimbo huo kumempa mafanikio na kuwa wimbo wa kwanza alioutayarisha kushika namba moja kwenye chart za Billboard 100.
Katika mahojiano yake ya hivi karibuni Billboard News alisema ilikuwa ndoto yake ya miaka mingi kufanya kazi na Kendrick.
"Ninaendelea kusema na siwezi kusema vya kutosha. Nitafanya nini ili niwe kwenye nafasi za juu? Nilikuwa nataka kusikia jina la Mustard tena wimbo utoke ukiwa na jina langu kama mtayarishaji mkuu.
"Kabla sijatengeneza wimbo wa 'Not Like Us',ilifika wakati nilikuwa natuma beats tano kwa siku ndani ya miezi mitatu hivi, ”alisema Mustard.
Alisema Kendrick alichagua beat moja ya Not Like Us na kumtumia verse mtayarishaji huyo ndipo alitengeneza wimbo huo.
"Huu ndio wimbo mkubwa zaidi ambao nimewahi kuwa nao maishani mwangu, Nilitaka tu wimbo na Kendrick,” alisema Mustard.
Hata hivyo, DJ Mustard alihusika kutayarisha nyimbo mbili kwenye albamu ya Kendrick Lamar ya 'GNX' iliyotoka 2024 ambazo ni 'TV Off' na 'Hey Now'. Nyimbo zote mbili ziliingia kwenye 10 bora ya chati ya Billboard Hot 100 na albamu ilishika nafasi ya kwanza kwenye Chati ya Albamu 200 za Billboard.

Leave a Reply