Aoa mara 53 kutafuta mwanamke wa kumpa furaha

Aoa mara 53 kutafuta mwanamke wa kumpa furaha

Asma Hamis

Mwanaume mmoja kutoka nchini Saudia aliyefahamika kwa jina la Abu Abdullah (63) amedaiwa kuoa mara 53 kwa kipindi cha miaka 43 kumtafuta mwanamke atakaeweza kumpa utulivu, furaha na amani kwenye Maisha yake, huku ndoa moja ikidumu kwa usiku mmoja tu.

Kwa mujibu wa tovuti mbalimbali nchini humo zinaeleza kuwa alioa kwa mara ya kwanza akiwa na umri wa miaka 20 na hakuwa na mpango wa kuongeza mke mwingine, lakini baada ya changamoto kuanza ndani ya ndoa ndipo alioa tena akiwa na miaka 23.

Licha ya Abdullah kuwa na ndoa mbili bado hakuwa akipata furaha aliyoihitaji kutoka kwa wake zake, hivyo aliamua kuoa tena mke wa tatu na wanne kwa mpigo, lakini hali iliendelea kuwa tete na kuamua kuwataliki wake zake wawili wa mwanzo.

Aidha hali hiyo ya kuoa na kuacha iliendelea kwa mwanaume huyo na kufikisha idadi ya wanawake 53, kupitia moja ya mahojiano yake alieleza hakuwahi kuoa kwa matamanio bali kwa lengo la kupata mwanamke atakaye mpa furaha, utulivu na Amani siku zote za maisha yake.

“Kila mwanaume duniani anataka kuwa na mwanamke mmoja na kubaki naye milele. Utulivu haupatikani kwa mwanamke kijana, bali kwa mwanamke mzee sikuwahi kuoa kwa matamanio binafsi bali kwa lengo la kupata Amani ya moyo wangu” alisema Abdullah,

Kwa sasa Abdullah ametajwa kuoa mwanamke mmoja tu na hana mpango wa kuachana nae wala kuongeza mwingine.






Comments 1


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags