Ariana Grande aumizwa na wanaokosoa mwonekano wake

Ariana Grande aumizwa na wanaokosoa mwonekano wake

Mwanamuziki na mwigizaji wa Marekani Ariana Grande amefunguka jinsi anavyoumizwa na baadhi ya mashabiki wanaojadili mwonekano wake.

Wakati akiwa kwenye moja ya mahojiano na mwigizaji mwenzake wa Wicked, Cynthia Erivo, Grande alijizuia kulia kutokana na mashabiki kukosoa mwili na nywele zake huku akiweka wazi kuwa mabadiliko hayo yanatokana na uhusika aliyocheza kwenye filamu ya Wicked.

“Nimesikia kila kitu. Nimesikia kila aina ya maoni kuhusu kile kinachodaiwa kuwa kibaya kwangu hasa kuhusu mwonekano wangu. Ni vigumu kujikinga dhidi ya kelele hizo, ni jambo lisilofurahisha bila kujali hisia unazopitia,”

“Hata ukienda kwenye chakula cha jioni cha Shukrani na bibi yako aseme, ‘Unaonekana mwembamba. Kulikoni? Unaonekana mnene. Kulikoni?’ Hilo ni jambo lisilopendeza na lenye maumivu bila kujali linapotokea na kwa kiwango gani linatokea.” Amesema Grande

Mwigizaji huyo mwenye umri wa miaka 31 ameweka wazi kuwa ilimbidi abadili mwonekano kufuatia na filamu hiyo inayoendelea kufanya vizuri ambapo ilimtaka kuwa mwembamba kiasi na kuwa na nywele za rangi ya dhahabu






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags