Aziz Ki, Hamisa kufunga ndoa Jumapili

Aziz Ki, Hamisa kufunga ndoa Jumapili

Nyota wa soka wa klabu ya Yanga Stephane Aziz Ki na mjasiriamali Hamisa Mobetto wameendelea kuibua mijadala kwenye mitandao ya kijamii, baada ya kuchapisha video zikidai wawili hao wanatarajia kufunga ndoa hivi karibuni. Kupitia ukurasa wa Instagram wa mtangazaji Zamaradi Mketema ameweka wazi kuhusu kuwepo kwa ndoa ya wawili hao, kwa kuchapisha bango lenye maelezo huku akiwapongeza. Katika chapisho hilo linaeleza kuwa Februari 15,2025 itakuwa siku ya kupokea mahari, Februari 16 Nikkah (ndoa) na Februari 19 ndiyo itafanyika sherehe ya wawili hao.

Utakumbuka hivi karibuni Hamisa na Aziz walionekana wakila bata pande za Dubai. Mbali na hayo hivi karibuni mama yake Hamisa wakati akizungumza na Mwananchi alikanusha taarifa za binti yake huyo kuolewa na mchezaji huyo.

"Kiukweli mimi hapana, sijui habari za ndoa wala sijapokea posa ya huyo mchezaji, mie nasikia tu kama unavyosikia wewe na kuona kwenye mitandao, nami ndiye mama mzazi na Hamisa, na mwanangu huwa hanifichi kitu chochote, tumezoea kuzungumza kila wakati na kupeana ushauri wa mambo mbalimbali, ila kwa hili kama lipo ningelijua tu,"alisema mama yake Hamisa.

Licha ya mama Hamisa kukanusha madai hayo jana Februari 9,2025, Mange Kimambi alichapisha video ya Hamisa na Aziz na kuisindikiza na maneno haya, "Na ikawe heri mdogo wangu, as long as you are happy na sisi tunaokupenda lazima tukusapoti, hakuna namna ❤️," aliandika Mange. Katika andiko hili Hamisa hakukanusha taarifa badala yake alikomenti emoji ya shukrani na kopa "❤️🙏🏽"






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags