Baada ya kucheza filamu zaidi ya 160, Michael Caine astaafu kuigiza

Baada ya kucheza filamu zaidi ya 160, Michael Caine astaafu kuigiza

Muigizaji mkongwe kutoka nchini  Uingereza Michael Caine ambaye  aliye wahi kuigiza filamu zaidi ya 160 atangaza kustaafu sanaa yake ya uigizaji kutokana na umri wake.

Michaeli anaeleza kuwa huu ni wakati sahihi wa yeye kustaafu ili aendelee na maisha mengine kwani  kipindi hichi hana mengi katika uigizaji.

Mike  mwenye umri wa miaka 90 anadai kuwa sasa hivi anataka kukaa na wazee wenzake ili aweze kuunda maisha yake mengine ya uzeeni akiwa katika mazingira ya kawaida bila kuhangaika na Sanaa.

Hata hivyo mapema mwaka huu aliweza kutoa filamu yake ya mwisho ambayo imetambulika kama ‘The Great Escaper’ amedai hiyo filamu ndiyo imekuwa alama yake ya mwisho katika sanaa.

Mike anasema ingawa anastaafu kuigiza lakini bado ataendelea kuandika stori za filamu na riwaya ambayo sasa anaifanyia kazi na anatarajia kuitoa Disemba mwaka huu.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags