Baadhi ya mawazo ya kibiashara kwa wanafunzi vyuoni

Baadhi ya mawazo ya kibiashara kwa wanafunzi vyuoni

Kama mwanafunzi, unaweza kuwa na muda mwingi wa kujihusisha na shughuli za ujasiriamali. Kuna fursa mbalimbali za kibiashara ambazo wanafunzi wa vyuoni wanaweza kuanzisha bila gharama kubwa ya mwanzoni au kuhitaji kutenga muda mwingi sana.

Maelfu ya wanafunzi wanajichumia mapato kupitia biashara ndogo zenye faida kubwa. Haya hapa ni baadhi ya mawazo ya biashara nzuri kwa wanafunzi

  • Kufungua mgahawa( cyber cafe)

Hili ni wazo la biashara la kwanza kabisa ambalo litakusaidia kupata kipato ukiwa chuoni ili biashara yako ikuwe Zaidi basi tafuta eneo ambalo liko karibu na chuoni kwenu ili uweze kujua biashara yako inavyotoka.

Kuna baadhi ya wanafunzi wakishafika chuon wanajiita slay queen wanaogopa kufanya biashara kisa watu watamuonaje, hayo ni maisha yako ndugu yangu usiogope wala kuangalia nani kasema nini fanya mambo yako na watu hawajui tuu biashara hii ina faida sana pale tu ukiwa serious nayo.

  • Kufungua duka la kuuza mavazi

Wanafunzi wa vyuoni wanapenda kuvalia nadhifu kwa mtindo wa kisasa, Biashara hii itakuwa na soko kubwa wakati wowote kwasababu wanafunzi wakishaingia chuo hupendelea Zaidi kila siku kuonekana akiwa tofauti mbele ya macho ya watu.

unahitaji tu kufanya utafiti wa mavazi yanayovuma kimtindo na upo tayari kwa biashara hii siku zote wanasema biashara ni moyo, Unahitaji kuwa na duka lililopo katika eneo la karibu na kupata fedha za kutosha ili uweze kuwa na aina tofauti ya nguo na bidhaa za mitindo kutoka kwa wanamitindo mbalimbali.

Iwapo duka halipatikani, unaweza kuuza vitu yako katika eneo wazi, hasa nyakati za jioni. Kwa kufanya hivi utajihakikishia mtiririko wa mapato.

  • Biashara ya ususi

Biashara zinazowalenga wanawake hustawi vizuri, Duka la ususi ni biashara ya faida kubwa sana ambayo mwanafunzi wa kike anaweza kuanzisha. Ni biashara inayohitaji muda mwingi, na inakuhitaji kusawazisha kati ya masomo na biashara. Ili kuwa na wateja wengi, unahitaji kujua mitindo ya nywele inayotrend.

Cha kufanya tuu ni kutafta msichana mmoja wa kazi ambae utasaidizane nae pindi wewe utakapokuwa darasani unaendelea na masomo, jambo la msingi kabisa ni kuwashawishi wanafunzi wenzako wawe wanasuka katika saloon yako

  • Kufungua duka la wakala

Biashara ya wakala ni yenye ushindani sana Kama chuo unaposomea kuna idadi kubwa ya wanafunzi, kutakuwa na soko kubwa na biashara yako ina uwezo wa kustawi vizuri. Unaweza hata kuchukua fursa hiyo ya kibiashara kwa kuuza vocha, Hebu fikiria kupokea mapato ya kila mwezi kutoka kwa mojawapo ya kampuni husika hii biashara ni yenye faida sana.

Uzuri wa biashara hii si lazima ufungue kibanda bali unaweza kutuma na kutoa pesa ukiwa hata uko class kwasababu vifaa vyako utakuwa unatembea navyo kila sehemu, hii itakusaidia mwenyew kujua leo umeingiza kiasi gani na umetoa kiasi gani.

  • Kupiga picha

Kama unapenda kupiga picha, hii ni nafasi yako ya kupata pesa kutokana na shughuli hii. Unahitaji tu kamera, mwanga, vifaa vya kudhibiti mwanga na ujuzi wa kupiga picha. Unaweza kutumia wikendi kwa kupiga picha katika harusi, mikutano, na sherehe mbalimbali.

Unaweza pia kutoa huduma ya kupiga picha na kuziuza kwa familia na watu binafsi. Unaweza pia kuuza picha zako kwenye soko la mtandao kama vile AfricanStockPhoto. Pia unaweza kupata pesa kupiutia wanafunzi wenzio kwa kuwapiga picha.

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags