Shenseea Ashushwa Jukwaani Kisa Vurugu Kenya

Shenseea Ashushwa Jukwaani Kisa Vurugu Kenya

Msanii kutoka Jamaica, Shenseea alilazimika kukatisha show na kushushwa jukwaani baada ya kuzuka vurugu katika tamasha la RahaFest lililofanyika usiku wa kuamkia Leo nchini Kenya.


Kwa mujibu wa tovuti mbalimbali zinaeleza kuwa vurugu hizo zilianzishwa na mashabiki ambao walikuwa wakilazimisha kuingia kwenye show hiyo bila ya tiketi hali ambayo ilipeekea polisi kuanza kurusha mabomu ya machozi kuwatawanya na show hiyo kuharibika.

Mbali na sababu hiyo lakini pia baadhi ya wadau waliweka wazi kuwa vurugu hizo
zilikuwa za maandamano kutokana na mchafuko uliopo nchini humo.

Inaelezwa kuwa Shenseea alitumbuiza kwa takribani dakika 7 tu na kushushwa jukwaani kwaajili ya kulinda usalama wake, hata hivyo msanii huyo kupitia ukurasa wake wa X (zamani Twitter) ameonesha kutopendezwa na vurugu hizo ikiwa ni show yake ya kwanza nchini humo.

Alikiba kutokea Tanzania ni miongoni mwa mastaa waliopanda kwenye jukwaa hilo la RahaFest lakini kwa upande wake show ilienda poa licha ya mabomu ya machozi kupigwa muda mchache baada ya Shenseea kupanda stejini.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags