Gavana wa zamani wa Lagos, Bola Ahmed Tinubu, ataapishwa leo kuwa rais mpya wa Nigeria. Hii inafuatia na uchaguzi uliokumbwa na utata mwezi Februari ambao unapingwa na upinzani mahakamani.
Huu ndio wakati Bola Ahmed Tinubu amekuwa akiusubiri katika kipindi chake chote cha kazi, na hatimaye ataapishwa kama kiongozi wa uchumi mkubwa zaidi barani Afrika.
Rais Tinubu akishika madarakani ya Muhammadu Buhari ambae ametetea kiti hicho kwa miaka minane ya uongozi wake.
Wakati wa hotuba iliyorekodiwa kwenye televisheni siku ya Jumapili, Buhari alidai kuwa anaondoka nchini humo akiwa katika hali nzuri kuliko alipoingia madarakani kwa mara ya kwanza.
Hotuba hiyo imekabiliwa na ukosoaji mkubwa kutoka kwa raia wa Nigeria, ambao wanalalamika juu ya ongezeko la gharama za maisha, pamoja na ukosefu wa usalama, chini ya utawala wake.
Maelfu ya watu wameondoka nchini humo kutokana na hali hiyo, huku raia wa Nigeria sasa ni miongoni mwa wapokeaji wakubwa wa viza nchini Uingereza, kwa mujibu wa takwimu za uhamiaji zilizochapishwa wiki iliyopita
Bola Tinubu atakabiliwa na shinikizo la kuonesha kwamba anaweza kugeuza hali ya nchi haraka.
Lakini kutokana na kwamba amedai kuwa alikuwa na mchango mkubwa katika kumfanya Buhari achaguliwe, baadhi ya watu wana wasiwasi kuwa huenda kipindi chake cha uongozi kisiwe cha kuleta mabadiliko nchini humo.
Huku baadhi ya viongozi kutoka katika mataifa mbalimbali wanatarajiwa kuhudhuria katika sherehe za kuapishwa kwa rais huyo akiwemo rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, Cyril Ramaphosa, Evariste Ndayishimiye na wengineo ambao wanaendelea kuwasili katika sherehe hizo.
Leave a Reply