Mcharazaji gitaa maarufu nchini aliyewahi kuzipigia bendi mbalimbali ndani na nje ya nchi, ikiwemo Extra Bongo '3x3', Ismail Kwembe a.k.a Bonzo Kwembe, amefariki dunia leo.
Akizungumza na Mwanaspoti, Dotto Manganje 'Mtoro wa Ulaya' ambaye anamuita Bonzo, baba mdogo amesema, mpiga gitaa huyo alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kisukari hadi kifo kikamkuta.
“Bonzo amefariki ssubuhi ya leo Jumamosi baada ya kuzidiwa na kupelekwa Hospitali ya Palestina, iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam, alikuwa anasumbuliwa na kisukari na mwili wake kwa sasa umehifahdhiwa Hospitali ya Mwananyamala,” alisema Manganje
Aidha aliongezea kwa kusema kuwa taratibu za mazishi zikiendelea kuandaliwa na msiba uko nyumbani kwa baba wa marehemi eneo la Mabibo Mwisho na kwamba mazishi ya mwanamuziki huyo huenda yakafanyika kesho eneo la Boko Mnenela, wilayani Kibaha yalipo makaburi ya familia.
Enzi za uhai wake, Bonzo Kwembe aliwahi kutamba na bendi kadhaa ikiwamo Mchinga Generation, Extra Bongo awamu ya kwanza Jibal Band na 'The Bokwe Tunes Band' aliyokuwa akiimiliki na kufanya shoo nje ya nchi.
Leave a Reply