Celine Dion achukizwa na Trump kutumia wimbo wake

Celine Dion achukizwa na Trump kutumia wimbo wake

Timu ya mwanamuziki Celine Dion imeoneshwa kukerwa na mgomea wa Rais wa Marekani, Donald Trump kwa kutumia moja ya wimbo wa msanii huyo kwenye kampeni iliyofanyika jijini Montana, mwishoni mwa wiki iliyoisha.

Utakumbuka kuwa juzi wakati wa mkutano wa kampeni, waandaaji wa hafla hiyo waliweka wimbo wa Dion uitwao ‘My Heart Will Go On’ ngoma ya mwaka 1997 iliyotumika katika filamu ya ‘Titanic’.

Timu ya msanii huyo imeonesha kukerwa na tukio hilo ambalo baadhi ya mashabiki walifikiria tofauti ambapo kupitia akaunti ya Celine ya X (zamani Twitter) ilitolea ufafanunuzi suala hilo kwa kuweka wazi kuwa wagombea hao hawakupewa idhini kutumia wimbo huo.

“Timu ya usimamizi ya Celine Dion na lebo ya ‘Sony Music Entertainment Canada’ inatoa taarifa kuwa matumizi ya kuchezwa kwa wimbo wa ‘My Heart Will Go On’ kwenye kampeni ya Donald hayajaidhinishwa kwa njia yoyote ile, hivyo basi timu inalifanyia kazi suala hili kukomesha tabia za wagombea kutumia kazi za wasanii bila idhini” imesema taarifa

Hii sio mara ya kwanza kwa Celine Dion kuonesha kupingana na Trump kwani mwaka 2017 msanii huyo aliwahi kukataa ombi la Trump la kumtaka atumbuize kwenye sherehe yake ya kuapishwa, vile vile pia mwaka 2020 aliwahi kukataa muziki wake usitumike kwenye kampeni zake.

Celine Dion sio msanii wa kwanza kukataa muziki wake usitumike kwenye harakati mbalimbali za Trump, wapo ambao walilipinga wazi akiwemo Bruce Springsteen, Neil Young, Tom Petty, Leonard Cohen na The Rolling Stones.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags