Cravalho: Moana imebadilishia maisha yangu

Cravalho: Moana imebadilishia maisha yangu

Mwigizaji wa Marekani Auli’i Cravalho, ambaye amejizolea umaarufu kupitia filamu ya ‘Moana 1 & 2’ amefunguka kuwa filamu hiyo imemfungulia maisha kwani imemuwezesha kumnunulia mama yake nyumba.

Cravalho aliyasema hayo alipokuwa akifanyiwa mahojiano baada ya uzinduzi wa filamu hiyo uliofanyika Novemba 27,2024.

“Tuliishi kwenye chumba kimoja cha kulala huko Mililani nilipochaguliwa kwa ajili ya filamu. Nililala chumbani, mama yangu alilala kwenye kochi. Alinipa kila kitu, zawadi pekee niliamua kumnunulia ni nyumba na naona sasa amestaafu kwa furaha, Moana imeniondolea umaskini," alisema Cravalho

Kwa mujibu wa tovuti ya ‘Business Insider Africa’ imeeleza kuwa filamu hiyo ilikusanya dola 643 milioni kimataifa katika mauzo ya tiketi, na mwendelezo wake, uliozinduliwa hivi karibuni unadaiwa kukusanya takribani dola 386 milioni ndani ya siku chache.

Cravalho binto mwenye umri wa miaka 24 amewahi kuonekana katika filamu za kawaida na animation zikiwemo Crush, The Little Mermaid Live, Darby and the Dead, Mean Girls, Moana 1&2 na nyinginezo






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags