Darasa kutoa Msaada kwa watoto mitaani

Darasa kutoa Msaada kwa watoto mitaani

Star wa HipHop nchini Tanzania Darasa @darassacmg225 leo Agosti 25, 2021 katika ukurasa wake wa Instragram ame-share clip ya wimbo wake mpya alio mshrikisha Abby chams @abby-chams na kuambatanisha ujumbe ulioeleza kuwa asilimia ya 70 ya ngoma hiyo itatumika kutoa misaada kwa watoto wenye uhitaji.

Darasa aameandika “Mauzo au mapato kutoka digital platform na chanzo chochote cha kuingiza pesa kupitia wimbo huu 70% zitasaidia kwenye vituo vya watoto wenye uhitaji (orphanage)”

Ameongeza kwa kusema “Hii ni program endelevu lengo ni kusaidia, kujenga jamii yetu, kuboresha na kusaidia watoto watoke mitaani ili tusipoteze nguvu ya kujenga taifa “ amemalizia kwa kusema we’re CMG kwenye Mungu tuna Amini  na kwenye kazi tunapigania amiin”






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags