Darassa amvulia kofia Marioo

Darassa amvulia kofia Marioo

Mwanamuziki anayetamba na ngoma ya ‘My Time’ Darassa amempa Marioo maua yake kufuatia na album yake iitwayo ‘The God Son’ inayotarajiwa kuachiwa leo Novemba 29, 2024.

Katika ukurasa wa Instagram wa Darassa amechapisha kava la album hiyo huku akiambatanisha na ujumbe wa pongezi kwa Marioo.

“Watu kama wewe na mimi, hakuna kinachoweza kutuondoa kutoka kazini. Na tutafanya kazi popote pale. Wewe ni mtu mchapakazi @marioo_tz, nakupa heshima hiyo, na najivunia sana kila wakati. Endelea kuwa halisi! Chapati maharage ni wimbo wangu” ameandika Darassa

Utakumbuka kuwa siku ya jana Marioo alifanya party ya kuzikilizwa kwa album hiyo huku ikihudhuriwa na mastaa mbalimbali akiwemo Harmonize, Jaivah, Ay, Joh Makini, Billnass, Zombie na wengineo.

Album hiyo ya pili kwa msanii huyo itaachiwa leo muda wowote katika mitandao ya kuuza muziki nchini ikiwa na ngoma kama Unanchekesha, Hakuna Matata, 2025, Salio, na nyinginezo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags