Diddy agonga mwamba kwenye dhamana, jaji adai usalama mdogo

Diddy agonga mwamba kwenye dhamana, jaji adai usalama mdogo

Ombi la dhamana la mkali wa hip hop Marekani Diddy Combs imekataliwa huku jaji wa mahakama hiyo akidai kuwa hawezi kumuachia huru rapa huyo kutokana na usalama kuwa mdogo kwa mashahidi.

Utakumbuka kuwa wiki iliyokwisha familia ya Combs ikiongozwa na watoto wake ilifika mahakamani kwa ajili ya kuomba dhamana lakini jaji Arun Subramanian, amekataa kutoa dhamani akisisitiza kuwepo kwa usalama mdogo kwenye jamii.

“Kutokana na asili ya madai katika kesi hii na taarifa zilizotolewa na serikali, mahakama inatilia shaka ukamilifu wa masharti yoyote yote yaliyoletwa na wanasheria wa Combs kama kikosi cha usalama tutupilia mbali ombi la dhamana hiyo kutokana na usalama kuwa mdogo kwa jamii”, aliandika Subramanian

Kwa mujibu wa Fox News wanasheria wa Diddy walipeleka tena ombi la kuomba dhamana huku wakiwa na fedha taslimu dola milioni 50. Mpaka kufikia sasa hii inakuwa dhamana ya tatu kukataliwa na baadhi ya majaji wa mahakama ya New York kwa kudai kuwa Combs hawezi kuwaachiwa huru kwani serikali inaamini kuwa rapa huyo ni hatari kwa jamii.

Kwa sasa Diddy amezuiliwa katika gereza la MDC Brooklyn, Combs alikamatwa na kutupwa gerezani Septemba 16 jijini Ney York kwa makosa makubwa ya unyanyasaji wa ngono, usafirishaji haramu wa watu huku kesi yake ikianza kusikilizwa Me 5, 2025.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post