Diddy akifurahia maisha Wyoming

Diddy akifurahia maisha Wyoming

Wakati baadhi ya wadau wakisubiria mkali wa Hip-hop Diddy akamatwe kufuatia na shutuma zinazomkabili za unyanyasaji wa kingono, sasa msanii huyo ameonekana akiendelea kufurahia maisha uraiani ambapo alionekana kwenye mji wa kitalii wa Wyoming uliopo Marekani.

Kufuatia na video zinazosambaa mitandaoni zimemuonesha Combs akiwa na marafiki zake katika sehemu maarufu ya bahari yenye mawimbi makali akipiga kasia.

Utakumbuka kuwa Diddy amekuwa akiandamwa na kesi za biashara ya ngono na unyanyasaji wa kijinsia tangu Novemba mwaka jana huku aliyekuwa mtayarishaji wa kazi zake Rodney "Lil Rod" Jones akidai kuwa Combs alikuwa akiandaa sherehe za biashara ya ngono.

Aidha licha ya kufunguliwa kesi saba msanii huyo anaendelea kula bata uraiani kutokana na kutokuwa na ushahidi madhubuti wa kumtia nguvuni Combs huku baadhi ya mastaa akiwemo Suge Knight wakidai kuwa Diddy ni FBI.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags