Diddy apata mshtuko, awekwa chini ya uangalizi

Diddy apata mshtuko, awekwa chini ya uangalizi

Ikiwa wiki inaenda kukatika huku hatma ya rapa Diddy ikiwa bado haijajulikana mwanamuiziki huyo amewekwa chini ya uangalizi ili asijiue.

Kwa mujibu wa tovuti ya People imeeleza kuwa bado haijafahamika kama Combs ana nia ya kujiua lakini ametajwa kuwa katika hali ya mshtuko.

Mbali na hayo kufuatia taarifa iliyotolewa na chanzo kilichopo ndani ya gereza kinadai kuwa uangalizi huo wa kuzuiwa kujiua umechukuliwa kama tahadhari kwa msanii huyo.

Diddy ameswekwa kwenye gereza la Metropolitan lililopo Brooklyn, New York tangu akamatwe Jumatatu usiku katika moja ya hoteli iliyopo Manhattan.

Naye wakili wa Diddy Marc Agnifilo ameripotiwa kuomba Combs ahamishiwe katika gereza la Essex County, New Jersey lakini hakupatiwa majibu yoyote kwani uamuzi wa mwisho uko mikononi mwa Ofisi ya Magereza.

Timu hiyo ya wanasheria wa Combs bado inawasiwasi ikisema kuwa hali ya gereza hilo haifai kwa kizuizi cha kabla ya kesi huku wakibainisha kuwa takribani watu wanne wamejiua ndani ya miaka mitatu iliyopita huku mmoja akijiua hivi karibuni.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags