Mkali wa Hip-hop kutoka Marekani Diddy Combs ambaye amezuiliwa katika gereza la MDC Brooklyn, lililopo jijini New York ametajwa kuwa msanii aliyetafuta zaidi kwa mwaka 2024 kwenye mtandao wa Google.
Kwa mujibu wa TechCrunch jina la Diddy ndio limetafutwa zaidi duniani kote hii ni kutokana na kukabiliwa na tuhuma za unyanyasaji wa ngono, usafirishaji haramu wa watu huku kesi yake ikianza kusikilizwa Mei 5, 2025.
Combs alikamatwa kwa mara ya kwanza Septemba 16,2024 jijini New York katika moja ya hoteli iliyopo jijini humo, ambapo kabla ya kukamatwa nyumba zake zilipigwa msako na kukutwa na mafuta zaidi ya chupa 1000.
Katika orodha hiyo iliyoongozwa na Diddy, namba mbili imeshikwa na Usher, Linkin Park, Sabrina Carpenter, Justin Timberlake, Angela Aguilar, Drake Bell, Tracy Chapman, Dave Grohl, na mwisho akiwa Angelina Mango.
Utakumbuka aliyekuwa akiongoza kutafutwa katika mtandao huo kwa mwaka 2023 ni Cristiano Ronaldo. Hiyo ilitokana na kufanya kwake makubwa katika soka hadi kupelekea kushinda Tuzo ya Maradona kutoka Globe Soccer kama Mfungaji Bora kwa mwaka 2023 akiwa na magoli 54.
Leave a Reply