Dj khaled amtamani Rihanna, Awatuma mashabiki kufikisha ujumbe

Dj khaled amtamani Rihanna, Awatuma mashabiki kufikisha ujumbe

Mtayarishaji wa nyimbo kutoka nchini Marekani DJ Khaled amewataka mashabiki wake kumshawishi Rihanna kushiriki katika albumu yake mpya.

Mkali huyo mwenye umri wa miaka 48 ametoa maombi hayo kwenye kipindi cha Tonight Show kilichoandaliwa na Jimmy Fallon hivi karibuni.

"Nimemtumia Rihanna rekodi ambayo nataka aiweke. Nahitaji ninyi nyote mnisaidie kufikisha ujumbe kwake,” alisema.

Utakumbuka mwaka jana nyota huyo wa muziki alidai kwamba mwimbaji wa Nigeria aliyeshinda Grammy, Burna Boy naye ni miongo kwa watakaoshiriki katika albamu hiyo.

Album hiyo kwa DJ Khaled itakuwa ya 14 ambapo amewahi kutoa albumu kama, We The Best, Suffering from Success, God Did, Major Key, We Global, I changed A lot, Victory, Kiss The ring, na nyingine nyingi.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags