Fanya haya kuzuia wizi kazini

Fanya haya kuzuia wizi kazini

Na Aisha Lungato

Katika kila sehemu ambayo inamzunguko wa watu wengi lazima kutakuwa na tabia zinazofaa na zisizofaa, na kama tunavyojua sehemu kama kazini, chuo, shule. Kunakuwa na watu ambao kila mmoja na tabia yake aliyotoka nayo kwao.

Na sehemu zenye mkusanyiko wa watu zaidi ya 10 lazima yupo mmoja ambaye atakuwa na tabia tofauti na wengine, na leo kwenye segment ya kazi tumekushushia mada ambayo itakusaidia kuthibiti wizi mahala pa kazi.

Kwanza: Afisa rasilimali watu atatakiwa kutoa barua ya ukumbusho ambayo itakataza suala hilo kuwa halifai katika sehemu hiyo ya kazi na hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote ambaye atakiuka maagizo hayo, barua hiyo pia itatakiwa ijirudie kila baada ya mwezi kupitia Group la wafanyakazi au email zao.

Pili: Kuweka ulinzi imara katika eneo la kazi, ili kuepukana na hili inatakiwa kuongeza ulinzi madhubuti wakati wa kutoka, kuangalia  hata CCTV camera, kuhusiana na suala la wizi si wafanyakazi tu wenyewe kwa wenyewe wanaweza kuchukuliana vitu bali hadi wafanyakazi wa usafi katika ofisi yenu wanaweza kufanya hivyo.

So kuweka ulinzi wa kutosha kutasababisha watu wenye tabia hiyo kuwa na uoga wa kuchukua kitu ambacho siyo chake kwa kuogopa ‘Kamera’ na walinzi walioko nje ya geti la Kampuni yenu.

Tatu: Kutomuamini kila mtu, suala la kumuamini mtu haswa kwa Watanzania limeendelea kuwa jipu haswa ambapo wapo baadhi ya watu wanalizwa kwa wizi na watu ambao anawaamini, suluhisho jingine ni kuacha kumuamini rafiki ambaye umekutana naye kazini kwani huwezi jua tabia na malezi aliyolelewa.

Nne: Jitahidi kutoacha vitu vyako vya muhimu kazini, waswahili wanamsemo usemao ‘Macho yameumbiwa kutamani’ hivyo basi pindi utakapo acha kitu chako mahala pa kazi ambacho kinaweza kumpendeza mtu machoni mwake kuna uwezekano mkubwa wa kuondoka nacho, ukiwa unatoka kazini jitahidi kubeba vitu vyako vyote mfano saa, flash, miwani, na hata wapo wanaoacha pesa pia.

Tano: Jitahidi kuwa na kumbukumbu, unapokwenda kuripoti kuwa umeibia basi uwe umeibiwa kweli, kwa sababu huenda kitu unachosema umeibiwa labda kuna mtu umempa au umekiacha nyumbani, hii itasaidia sana kuepusha kuwaingiza watu matatizoni maana itakapo gundulika inaweza kusababisha ukafukuzwa kazini, kumbuka sehemu unayoweka na kuacha vitu vyako na watu unaowapatia.

Licha ya kuzungumza yote hayo lakini suala la udokozi linatakiwa likomeshwe kwa kuanzia na wewe mwenyewe, kama ulivyofanikiwa kuacha kufanya mambo mengine ambayo hayana msingi katika maisha yako basi na hili la udokozi pia unaweza kulikomesha kabisa.

Na ili uepukane na masuala ya wivu lazima uachane na tamaa ndogo ndogo, jitahidi kuridhika na hali ya maisha yako na pamoja na kipato unachokipata bila kusahau kumuomba Mungu aweze kukufanikisha kuachana na suala hilo, maana ukianza kwa kuiba leo tsh 100 kesho utaongeza na mpaka utafikia kuwa mwizi mbobevu.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags