Fei Toto ampongeza Aziz Ki

Fei Toto ampongeza Aziz Ki

Kiungo wa Azam FC, Feisal Salum 'Fei Toto' amempongeza Stephane Aziz Ki kwa kuibuka mfungaji bora kwa kupachika mabao 21 huku akiweka wazi kuwa alistahili.

Fei Toto ambaye amefunga mabao 19 akiachwa mabao mawili na kinara huyo ambaye walikuwa wanakimbizana kwenye ushindani, amesema licha ya kukosa kiatu cha dhahabu msimu huu anafurahi kuipambania ‘timu’ yake kushiriki ‘Ligi’ ya Mabingwa Afrika.

“Nampongeza Aziz Ki kwa kufanikiwa kutwaa kiatu cha dhahabu, alistahili kutokana na namna ambavyo amepambana, na mimi pia licha ya kukikosa ninafuraha kuipeleka Azam FC Ligi ya Mabingwa nafasi ambayo ndiyo ilikuwa katika malengo yetu msimu huu.

Haikuwa rahisi, nafurahi mimi pia pamoja na kuipeleka Azam FC kimataifa nilionesha ushindani kwenye mapambano ya kiatu, bahati haikuwa yangu kwani mchezo wa mwisho pia kafunga na mimi nimefunga lakini amekuwa bora kwa sababu yeye kafunga mabao matatu mimi nimefunga moja ambalo lilikuwa muhimu na la faida” amesema #FeiToto

#AzizKi amepokea kwa furaha pongezi kutoka kwa Fei Toto akimpa moyo kuwa msimu ujao watafanya kama walivyofanya msimu huu lakini kwa ubora zaidi.

“Msimu ujao tutafanya kama tulivyofanya msimu huu lakini kwa ubora zaidi nimefurahia namna ambavyo tulikuwa tunapeana changamoto kuelekea kutwaa kiatu cha ufungaji bora, Fei Toto ni rafiki yangu na huwa tunazungumza na ndiyo maana amenipongeza lakini nakubali kiwango chake na naheshimu kujituma kwake naamini hili litaendelea msimu ujao” amesema #Aziz.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags