Kwa mujibu wa tmz Netflix iko hatua za mwisho kupata hati ya kuonesha filamu hiyo iliyotayarishwa kwenye studio za Cent, ‘G-Unit’ baada ya kuzipiga chini baadhi ya Tv na mitandao iliyokuwa ikitaka kuionesha filamu hiyo kwa mara ya kwanza.
50 Cent akijibu kuhusu habari hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram ameeleza kuwa ili Netflix iweze kujihakikishia kuonesha filamu hiyo inabidi waathiriwa wajitokeze kwa wingi ili kuweza kupata vipindi zaidi.

Ikumbukwe kuwa habari ya filamu ya Diddy kuoneshwa Netflix inakuja muda mfupi baada ya kusambaa kwa video ikimuonesha Combs akimshambulia mpenzi wake wa zamani Cassie Ventura katika hoteli ya Los Angeles mwaka 2016.
Leave a Reply