Filamu Ya The Weeknd Kutoka Mei 16

Filamu Ya The Weeknd Kutoka Mei 16

Filamu ya mwanamuziki kutoka Canada, The Weeknd iliyopewa jina la ‘Hurry Up Tomorrow’ imeripotiwa kutoka na kuanza kuoneshwa katika kumbi za sinema Mei 16,2025.

Filamu hiyo ya kisaikolojia itawahusisha mastaa kama The Weeknd, Jenna Ortega, na Barry Keoghan. Filamu hiyo inahusiana na albamu ya sita ya The Weeknd yenye jina hilo hilo na inahusu mwanamuziki anayekumbwa na kukosa usingizi na matatizo mengine.

Ikiandikwa kwa ushirikiano na kuzalishwa na Abel Tesfaye pamoja na mkurugenzi Trey Edward Shults, mradi huo unachunguza mada kuhusu afya ya akili na mabadiliko ya kibinafsi.

Ikumbukwe ujio wa filamu hiyo ya ‘Hurry Up Tomorrow’ ulitangazwa rasmi na kampuni ya ‘Lionsgate’ Novemba 4, 2024.

Albamu ya sita ya The Weeknd, ilitoka rasmi Januari 31, 2025, ikiwa na jumla ya nyimbo 22 huku mwanamuziki huyo akiwashirikisha mastaa wenzake mbalimbali wakimeo Anitta, Playboi Carti, Travis Scott, Florence Welch, Future, na Lana Del Rey.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags