Mwanamuziki na mfanyabiashara tajiri kutoka Guinea, Moussa Sandiana maarufu Grand P, amemtambulisha mpenzi wake mpya aitwaye Mariame, baada ya kuachana na mwimbaji na mwanamitindo kutoka Ivory Coast, Eudoxie Yao.
Kupitia ukurasa wa Instagram wa Grand P alishiriki picha na video akiwa na mpenzi wake huyo huku akionesha mapenzi makubwa na furaha kwa mpenzi wake huyo ambapo aliandika.
“Mabawa ya kuku wangu, Tazama jinsi walivyo wazuri asante, Bwana wewe ndiye chanzo cha furaha yangu, na sitamani chochote zaidi ya kuwa nawe kando yangu maishani. Njoo karibu na uufariji moyo huu ambao unauliza tu kutetemeka kwa mpenzi wako," ameandika Grand P
Utakumbuka kuwa msanii huyo alitrend kupitia mitandao ya kijamii kufuatia na uhusiano wake na mwanamitandao wa Ivory Coast, Eudoxie huku wakiachana mapema mwaka 2023, adiha kufikia Aprili mwaka huo huo alitambulisha tena mpenzi mwengine aitwaye Yubai Zhang na kuachana naye mwaka jana.

Leave a Reply