Hadhi ya vyuo vikuu iko wapi

Hadhi ya vyuo vikuu iko wapi

Na Leonard Musikula

Niajeee! Wanangu wa Mwananchi Scoop!

Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika moja ya falsafa zake juu ya uhuru na ujamaa alisema kuwa nafasi ya msomi mkubwa katika nchi zinazoendelea ni kuchangia mawazo, wafanyakazi na huduma chanya kwa ajili ya kuendeleza maendeleo ya watu.

Aidha, Chuo Kikuu kinatazamwa na jamii na serikali kuwa ni kiwanda kinachozalisha viongozi wasomi ambao kwa namna moja au nyingine wanaweza kulisaidia taifa kuondokana na umaskini.

Lakini hivi leo, vitovu vya taaluma vinakabiliwa na changamoto kubwa ya mmomonyoko wa maadili miongoni mwa baadhi ya wanafunzi ambao kwa kawaida hukerwa na maono ya uwepo wa taasisi hiyo na uhalisia wake.

Wanachuo wengi hubadilika kadri siku zinavyosonga ikiwa ni pamoja na kujishughulisha na shughuli zisizoendana na matakwa ya elimu waliyohudhuria katika taasisi hizo.

Kutokana na makundi rika pia, tabia ya baadhi ya wanafunzi kubadilika huku wengine wakidai inatokana na maisha magumu, lakini mianya hiyo inatokana na kuwepo kwa uhuru mkubwa ndani ya vyuo hivyo, kwa mujibu wa wataalamu.

Pengine haya pia yanaweza kuwekwa katika kundi la madhara ya utandawazi. Mitandao ya kijamii ipo ili kuwasaidia wanafunzi katika masomo na kazi zao, lakini wengine hutumia mitandao hii isivyofaa.

Uchunguzi uliofanywa na jarida la Success umebaini kuwa matumizi mabaya ya teknolojia hasa mitandao ya kijamii yamesababisha ongezeko la uhalifu, ubakaji, matumizi ya dawa za kulevya na kujiuza zaidi kwa baadhi ya wasomi wa vyuo hivyo.

Kumekuwa na matukio ya wazi ya hivi karibuni, hasa kwenye mitandao ya kijamii yanayosambaa bado yakiwaonyesha wanaojiita wanafunzi wa elimu ya juu wakiwa wamejirekodi wakifanya mapenzi au wakiwa nusu uchi bila aibu wala woga. Haya kiutamaduni hayana maadili na yanahitaji kukemewa zaidi na zaidi kulingana na pande zinazohusika.

Kufikia mwisho wa 2021, zaidi ya video mbili za ngono zilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii (Twitter, WhatsApp), ambazo ziliaminika kuwa zilihusisha wanafunzi wa vyuo vikuu nchini.

Mmoja wao ilihusisha vijana watatu wa chuo kimoja maarufu jijini Dar es Salaam ambao majina yao yamehifadhiwa, hata hivyo kilichowashangaza watu zaidi ni kile kilichoonyesha mwanafunzi wa kike anayesoma chuo kikuu kingine maarufu alipokuwa akijaribu kuingiza chupa ya soda kwenye sehemu zake za siri

Haya ni matukio yaliyoenea na kuzua tafrani katika jamii hasa kwa makundi yaliyoweza kushuhudia au kusikia matukio yaliyokuwa yakizungumzwa.

“Nilihuzunishwa sana na kitendo cha msichana aliyekua msomi kufanya vile. Hata dunia ikiharibika lazima kuwe na njia ya kudhibiti uhalifu huu,” alisema Benjamin Mussa, 60, mkazi wa Dar es Salaam. 

Hii ni mifano michache tu lakini kwenye mitandao bado kuna clip nyingi zinazohusisha wanafunzi wa elimu ya juu, zinazosambaa huku ikisemekana video hizo zinasambazwa na wanafunzi wenyewe.

Moja ya sababu zilizotolewa ni kwamba wanafunzi wanarekodi kwa ajili ya kuvutia wafuasi wengi katika kurasa zao za mitandao ya kijamii huku wengine wakifanya hivyo kujiingizia kipato.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Detricia Pamba

A Digital Journalist, Content Creation Executive at Mwananchi Communications Ltd and Chief Editor of Mwananchi Scoop. I'm also writes stories around Technology, every Wednesday on Mwananchi Scoop. My other famous segments on Mwananchi Scoop include LISTI and WHO’S HOT.


Latest Post

Latest Tags