Haji Manara Na Zaylissa Watimiza Mwaka Mmoja Wa Ndoa

Haji Manara Na Zaylissa Watimiza Mwaka Mmoja Wa Ndoa

Baada ya kuwepo na minong’ono mingi kuhusiana na ndoa ya aliyekuwa msemaji wa Yanga, Haji Marana na mwigizaji Zaylissa kutokufikisha mwaka, hatimaye wawili hao siku ya leo wanasherehekea mwaka mmoja wa ndoa yako.

Katika kusheherekea siku hiyo Haji ameandaa shughuli kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa ngozi inayofanyika leo Januari 24, 2025 Ocean Road jijini Dar es Salaam kwa lengo la kufurahia mwaka mmoja wa ndoa pamoja na siku yake ya kuzalia, ambapo alizaliwa Januari 18.

Ndoa hiyo si ya kwanza kwa Zaiylissa ikumbukwe kuwa mwaka 2023 alifunga ndoa na mwanamuziki wa singeli Dulla Makabila, na ndoa yao ilidumu kwa mwezi mmoja tu.

Kwa upande wa Haji pia siyo ndoa yake ya kwanza kwani aliwahi kufunga ndoa na wanawake kadhaa kama vile Rubynah, Rushaynah na Naheedah, na hii ni ndoa ya sita kwa Manara kufuatiwa na malezo ya mama yake mzazi wakati alipokuwa anafunga ndoa na Rushaynah.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags