Kwa mujibu wa ‘Hollywood Reporter’ nyimbo za marehemu Rapa Notorious B.I.G. zimewekwa sokoni kwa ajili kuuzwa kwenda kampuni ya ‘Primary Wave’ kwa dola 150 milioni ikiwa ni zaidi ya Sh 396 Bilioni.
Dili hilo la kuuza haki za muziki wake linakuja baada ya Mama yake mzazi Bi. Voletta Wallace, kufariki dunia Februari 21, 2025 ambapo mali zote za B.I.G. zilikuwa zinamilikiwa na kusimamiwa na mama huyo tangu mwaka 1997 baada ya kifo cha B.I.G.
Voletta Wallace alichukua jukumu hilo muhimu la kusimamia mali ya muziki wa Biggie pamoja na watoto wa msanii huyo ambao ni T’yanna Wallace (31)na C. J. Wallace (28).
Utakumbuka, Hii sio mara ya kwanza kwa msanii kuuza Katalogi au hakimiliki ya muziki wake kwani mwezi Februari, 2025 Mwanamuziki wa marekani T-pain aliripotiwa kuuza katalogi yake ya uchapishaji 'Hakimiliki ya muziki wake' pamoja na baadhi ya masters zake za muziki kwenye kampuni ya HarbourView Equity inayohusiana na uwekezaji katika ubunifu, na masuala ya vyombo vya habari.
Hata hivyo, dili hii ya B.I.G inatajwa kuwa miongoni mwa dili kubwa kwenye historia ya muziki wa Hip Hop.

Leave a Reply