Ni wazi kuwa mwanamitindo Hamisa Mobetto amegeuka mwalimu wa lugha kwa mumewe Stephanie Azizi Ki. Hiyo ni baada ya nyota huyo wa soka kuweka wazi kuwa amekuwa akifundishwa kiswahili na mkewe.
Nyota huyo wa klabu ya Yanga amesema hayo baada ya Hamisa kukanusha taarifa za baadhi ya watu zinazodai yeye ndiyo huusika katika kumuandikia mumewe maelezo kwenye machapisho yake ya mitandao ya kijamii, na kumtaka Aziz ajieleze mwenyewe.
"Naandikaga mwenyewe kapisheni natakiwa kujifunza na kuelewa kwa sababu natakiwa kuongea na familia ya mke wangu. Ninaye mwalimu wangu hapa (Hamisa) kila mara ananifundisha kwa hiyo ni muhimu sana kwangu kujua kiswahili,"amesema Aziz Ki.
Hata hivyo, Hamisa amewahakikishia mashabiki kuwa mpaka mwakani 2026 mumewe, atakuwa tayari anafahamu vizuri kiswahili
Utakumbuka Aziz ni ambaye ni raia Burkina Faso alifunga ndoa na Hamisa Februari 16, 2025, huku Februari 15, 2025, ikiwa ndiyo siku ambayo Hamisa alitolewa mahari ya ng'ombe 30 na kiasi cha Sh 30 milioni.

Leave a Reply