Harmonize hakuwa na kibali kurekodi Zanzibar

Harmonize hakuwa na kibali kurekodi Zanzibar

Sasa mambo hadharani!!! Yapata siku kadhaa zimepita tangu msanii Harmonize atuonyeshe kwenye mitandao ya kijamii kuwa yuko Zanzibar kwa ajili ya kushoot video za baadhi ya nyimbo zake, taarifa rasmi aliyotolewa leo ni kuwa amezuiwa na Baraza la Sanaa Zanzibar kufanya video katika mwezi huu Mtukufu wa Ramadhan.

Baraza la Sanaa Zanzibar limetoa tamko kuwa harmonize hakuwa na kibali cha kufanya video hiyo. Kufuatia mahojiano na moja ya chombo cha habari kisiwani humo Mrajisi wa Baraza la Sanaa Zanzibar, Juma Chuma Juma amesema kuwa
“Harmonize hakuwekwa Kituo cha Polisi, aliyewekwa Polisi ni meneja wake kwa kuwa alitueleza kila kitu kinachohusiana na msanii huyo ahojiwe yeye. Mamlaka hiyo ilitoa katazo lakini uongozi huo ulikaidi,” amesema.

Ameongeza kuwa, “Tulimkamata kwa kosa la kuvunja Sheria namba 7 ya mwaka 2015. Hii inaekeleza utaratibu wa kufanya kazi aina yoyote ndani ya Zanzibar. Hamornize alipaswa kuomba kibali maalumu kutoka kwa Baraza la Sanaa ili tukague na tujiridhishe,” amesema Juma.

Katika video mbalimbali zinazosambaa mtandaoni, zimemuonyesha Harmonize akiomba radhi kwa Wazanzibari kama kuna usumbufu wowote aliowasababishia, huku akiweka wazi kuwa hakupata tangazo kutoka Serikali ya Zanzibar kuhusu katazo la kushuti video kwenye kipindi cha mwezi huu Mtukufu wa Ramadhan.

Aidha mpaka sasa bado Baraza la Sanaa Zanzibar halijatoa kibali cha ruhusa kwa msanii Harmonize.

Chanzo the Chanzo media






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags