Harmonize kusaini wasanii wawili mwaka huu

Harmonize kusaini wasanii wawili mwaka huu

Mwanamuziki na mmiliki wa ‘lebo’ ya #Kondegang, Harmonize ameahidi ku-saini wasanii wawili mwaka huu katika ‘lebo’ yake hiyo. 

Harmonize kupitia ukurasa wake wa Instagram ameshusha ujumbe uliokuwa ukieleza kuwa alishakata tamaa ya kusaidia wasanii wenye uwezo lakini msanii wake #Ibraah amemshauri kuwa-sapoti wasanii wengine, ambapo Harmonize amedai kuwa mwaka 2024 atasaini wasanii wawili.

Aidha Konde Boy ametupa vijembe kwa wasanii ambao wameondoka katika ‘lebo’ yake hiyo kwa kueleza kuwa

“Nimekaa hapa nawatazama wale waliofanikiwa kuwatia ujinga Wasanii wengine ambao walikuwa @kondegang na kuwaaminisha watafanikiwa zaidii hata mimi wakati mwingine ilinibidi niamini hivyo ndio maana kwa Moyo mkunjufu nilizibariki safari zao ila chakusikitisha imekuwa ndivyo sivyo”. 

Ikumbukwe kuwa mpaka kufikia sasa wameshaondoka wasanii watatu katika ‘lebo’ ya #Kondegang akiwemo #Anjella, #Cheed na #Killy






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags