Harmonize: Platform hazijanilipa mauzo yangu

Harmonize: Platform hazijanilipa mauzo yangu

Huku mvua ya kutoa nyimbo ikiendelea kwa msanii Harmonize ameweka wazi kuwa kuna baadhi ya platform zinapopatikana kazi zake hazijamlipa mauzo yake.

Kupitia #InstaStory yake amefunguka hayo kwa kuandika ,

”KONDEGANG FC  taarifa ngoma zinazotoka leo hazitopatikana katika platform kadhaa kwa sababu zifuatazo,  hawajanipatia report ya mauzo yangu tangu january mwaka huu, sio mimi ni Konde gang yote kwa hiyo sijaona sababu za kuwapa nyimbo zangu zingine

Niwahahakishie tu serikali ya awamu ya sita ipo macho sana na imeahidi kutusaidia ikiambatana na kukomesha kabisa vitendo hivi vya unyonyaji, Wahindi tunalifuatilia kwa makini sana can you imagine I have never made even 1$ kupitia single again how big it is in the world,

 Wizara inalishughulikia kwa makini kushirikiana na COSOTA & BASATA mh. Waziri pamoja na Naibu Waziri my brother @mwanafa asante kwa ushirikiano”






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags