Baada ya kuwepo kwa minong’ono kwa baadhi ya watu kupitia mitandao ya kijamii ikidai kutoelewa jina la wimbo wa msanii wa Injili Joel Lwaga, ‘Olodumare’, hatimaye msanii huyo ametoa maana ya jina la wimbo huo kwa kueleza kuwa maana yake ni Mungu.
“Olodumare maana yake ni Mungu kwa Kiyoruba sio Mungu wa Kiyoruba ni kama vile Kyala kwa Kinyakyusa, Sehba kwa Kisukuma au Ruwa kwa Kichaga, Myoruba aliyemfahamu Mungu wa kweli na asiyejua kingereza wala lugha nyingine yoyote anamwita Mungu Olodumare,”
“Kwa upande wingine Myoruba anayeabudu miungu asiyejua kingeleza atamuita huyo Mungu wake Olodumare,” amesema Lwaga
Mbali na hayo ameeleza sababu ya kutumia lugha hiyo huku akiweka wazi kuwa lengo lilikuwa kuufanya muziki wa Injili kupenya Kimataifa.
“Lengo la kuchanganya Lungha ni kuweza kupenya na kuwafikia kirahisi mataifa mengine nje ya mipaka ya East Afrika, na neno la Olodumare sio geni kwenye nyimbo za injili za Nigeria hao wenye lugha yao ni geni kwetu. Watumishi wa Mungu wengi Nigeria wana nyimbo zinazoitwa Olodumare,” amemalizia
Yoruba ni lugha ya Niger-Congo inayozungumzwa Afrika Magharibi, hasa katika maeneo ya Kusini Magharibi na Kati mwa Nigeria ambapo wazungumzaji wa lugha ya Yoruba ni takribani milioni 47 huku watu milioni 2 wakiitumia kama lugha ya pili, baadhi ya sehemu ambapo lugha hiyo hutumika ni pamoja na Nigeria, Benin, na Togo, pamoja na jamii ndogo za wahamiaji nchini Côte d'Ivoire, Sierra Leone, na Gambia.
Leave a Reply