Baada ya kuripotiwa kwa taarifa za kifo cha mwigizaji maarufu Kim Sae-ron (24) aliyefariki dunia nyumbani kwake jijini Seoul, hatimaye sababu kifo chake imetambulika.
Kwa mujibu wa vyombo vya usalama nchini humo, vinaeleza kuwa mwigizaji huyo amefariki dunia kwa kujiua, “Tunaamini alichukua uamuzi wa hali ya juu na tunapanga kulishughulikia kama kesi ya kujiua,” imeeleza taarifa hiyo.
Hata hivyo kwa mujibu wa vyombo vya habari mbalimbali nchini humo vinaeleza pia mwigizaji huyo hakuacha barua yoyote kuhusiana na kujiua kwake.
Kim alizaliwa Julai 31, 2000, na alifariki dunia Februari 16,2025 mwili wa msanii huyo uligundulika na rafiki yake aliyemtembelea nyumbani kwake. alianza safari yake ya sanaa akiwa na umri wa miaka tisa kupitia filamu A Brand New Life (2009), ambayo ilimpatia umaarufu mkubwa.
Aidha aliendelea kung’ara zaidi kupitia filamu The Man from Nowhere (2010), ambayo ilimfanya kuwa miongoni mwa waigizaji chipukizi wenye mvuto mkubwa katika tasnia ya filamu ya Korea Kusini.
Katika miaka iliyofuata, alishiriki katika filamu zingine kubwa kama ‘A Girl at My Door’ (2014) na tamthilia za televisheni zikiwemo ‘Secret Healer na Leverage’.

Leave a Reply