Katika familia hiyo wote ni watu wa kujishughulisha na pia ni watu ambao wanamiliki ‘Brand’ kubwa za vitu mbalimbali, tukianza na chapa maarufu ya ‘Skims’ inayomilikiwa na Kim Kardashian ilianzishwa mwaka 2009 na imekuwa na mafanikio makubwa ambayo inadaiwa kufikia zaidi ya dola 3.2 bilioni.

Ukiachilia mbali Kim kuna Kylie Jenner mwanadada anayemiliki vipodozi vya ‘Kylie Cosmetics’ vinadaiwa kifikia thamani ya zaidi ya dola milioni 600, vilevile kwa Kourtney Kardashian na chapa yake ya ‘Poosh’ yenye thamani ya dola 15 milioni.
‘Good American’ kutoka kwa Khloe Kardashian inayokadiriwa kuwa na thamani ya dola 12 milioni, yupo Kendall Jenner na chapa yake ya ‘818 Tequila’ ambayo ilitambulishwa mwishoni mwa mwaka 2023 chapa ambayo bado haina mafanikio zaidi, huku wadau wakidai kuwa ni kutokana na mwanadada huyo kugoma kutumia jina la famila katika chapa hiyo.
Kris Jenner ambaye anamiliki chapa ya bidhaa za usafi za kusafishia mikono na vyombo iitwayo ‘Safely’ ambayo inapatikana katika mtandao wa Amazon inadodaiwa kuuzika sana nchini Marekani.
Leave a Reply