Ibrah anogewa na singeli, aja na Kwani We Nani Remix

Ibrah anogewa na singeli, aja na Kwani We Nani Remix

Baada ya mwanamuziki wa Bongo Fleva nchini Ibrah kuweka wazi kuwa yupo tayari kuwekeza nguvu katika muziki wa Singeli, hatimaye msanii huyo ameonesha nia yake hio kwa kutoa singeli nyingine ya kufungia mwaka.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa msanii huyo ameshare kipande cha singeli iitwayo ‘Kwan we Nani” aliyoshirikishwa na Meja Kunta, Jay Combat huku ikishika nafasi ya 12 katika mtandao wa YouTube ikiwa na siku moja tuu tangu kuachiwa kwake.

Ikumbukwe kuwa Ibraa baada ya kupokelewa kwa ukubwa kupitia singeli ya ‘Wivu remix’ aliweka wazi kuwa ifikapo mwaka 2025 atawekeza zaidi katika muziki huo na kuwataka wasanii wa singeli wamuache kidogo.

“Nimenyoosha mikono juu huu wimbo umenifanya niamini kuwa wa Tanzania tunapenda sana music wetu wa singeli na ahadi yangu nitazidi kuwekeza zaidi kwenye music wa singeli 2025 kauli mbio yetu itakuwa ni singeli kwanza wasanii wasingeli acheni utani na kazi yangu,” aliandika Chinga

Hii ni singeli ya tatu kwa Ibrah kushirikishwa na kufanya vizuri, Utakumbuka kuwa mwaka 2021 alishirikishwa katika singeli ya ‘Do Lemi go’ na Kinata Mc, ikaja Wivu na sasa ‘Kwani we nani’ ambazo zote kwa pamoja zinaendelea kukimbiza katika mtandao wa YouTube.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags