Iggy akatisha show baada ya suruali kuchanika jukwaani akitumbuiza

Iggy akatisha show baada ya suruali kuchanika jukwaani akitumbuiza

Mwanamuziki kutoka Australia Iggy Azalea wakati akitumbuiza kwenye tamasha Boulevard Riyadh City nchini Saudi Arabia, alilazimika kukatiza show jukwaani baada ya suruali aliyokuwa amevaa kuchanika.

Iggy alikuwa amevaa suruali ya kubana yenye material ya mpira, nguo hiyo ilichanika upande wa paja la kushoto wakati akicheza style ya kupiga magoti chini na kuacha paja lake wazi, kitendo kilichofanya azuiliwe kuendelea na utumbuizaji wake kwani sehemu ya mwili ilikuwa wazi.

Rapper huyo wa Australia licha ya kupatwa na tukio hilo jukwaani ameonesha kutoa shukurani zake za dhati kwa baadhi ya mashabiki na waandaaji wa tamasha kwa kumuonesha upendo licha ya nguo yake kuchanika na kupelekea kukatiza show hiyo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags