Jackson Nyamambaya: kazi ya content creator imevutiwa na mimi

Jackson Nyamambaya: kazi ya content creator imevutiwa na mimi

Kujiongeza na kujitambua, kujituma ndiyo mambo makuu matatu yatakayomsaidia kijana kuhakikisha anafanya kile ambacho amekikusudia kwenye maisha yake.

Nikwambie tu kwa miaka ya hivi karibuni ili uweze kupiga hatua katika maisha lazima ustrugle kadri unavyoweza na kujitoa zaidi katika kuhakikisha unafika safari yako ya mafanikio.

Jackson Nyamambaya maarufu kama Jackie8 ni kijana anayefanya kazi ya content creator aliyejikita zaidi kwenye masuala ya Comedy.

Nyamambaya pia ni Mwanafunzi kutoka Chuo cha IFM akiwa mwaka wa tatu chuoni hapo akichukua course ya Insurance in social protection.

Akizungumza na jarida la Mwananchi Scoop Jackie8 amefunguka mambo mbalilmbali ikiwemo namna anavyoichukulia kazi hiyo, nini hasa kimemvutia pamoja na changamoto anazozipitia.

Akielezea namna anavyoichukulia kazi hiyo Jackie8 alisema awali alikuwa anafanya kwa funny tu, kutokana na ucheshi wake aliokuwa nao  ila baada yakuanza kutengeneza content ndipo alipogundua umuhimu mkubwa wa kazi hiyo.

Aidha alisema kwa sasa anaichukulia ni professional kabisa na yuko very serious kwa kile anachokifanya kwani ndiyo kazi inayoendesha maisha yake kwa sasa na anaiheshimu pia.

Vilevile alisema kazi hiyo inahusisha kipaji na uwezo uliokuwa nao katika kuhakikisha unaandaa maudhui ambayo yatawavutia watazamaji au wasikilizaji kwa kile ambacho unakipresent kwao.

Pia alisema binafsi yake yeye anafanya kazi hiyo wala haihusiani kabisa na masomo anayosoma chuoni lakini kutokana na uwezo wake wa kuandaa content ndiyo unaomsaidia kwenye kufanya vizuri kazi zake.

Hata hivyo alizungumzia ugumu na changamoto mbalimbali ambazo anazipitia wakati akiwa anafanya kazi hiyo ikiwemo Vifaa vinavyotumika kwenye kushoot clip mbalimbali.

“Kiukweli changamoto nyingi sana kwanza vifaa vya kutumia kwenye kushoot kama camera hivyo unakuta tunatumia simu, bado materials sometimes unakuta video inahitaji gari wewe huna lakini pia bado binadamu hawajakukatisha tamaa kwa maneno ya kukukosoa hivyo inavigingi vingi sana”alisema.

Aidha alisema kazi hiyo ndiyo imevutiwa na yeye jambo ambalo limesababisha kuipenda zaidi kutokana na ucheshi aliokuwa nao.

Vilevile alisema kazi hiyo inambeba kwani tayari ameshaanza kuona matunda yake.

“Sihaba Mungu sio Athumani mwanzo ilkua hainisapoti lakini kuanzia mwaka jana hadi mwaka huu nimeanza kupata matangazo mbalimbali ambayo yananisaidia maisha yasonge”

Hata hivyo alisema kipaumbele chake kikubwa kwenye maisha yake ni kazi ambayo anaifanya ndiyo kitu kikubwa akimtoa Mungu pamoja na wazazi wake.

Aidha Jackie8 kwenye maisha ya kawaida tofauti na kazi anayoifanya alisema yeye ni mtu mpole, na mcheshi ambaye hapendi kusemewa vibaya kuhusu kazi ambayo anaifanya.

Hata hivyo alizungumzia Mavazi pamoja na viatu anavyopenda kuvaa nje ya kazi zake alisema anavutiwa zaidi na vazi la Tshirt pamoja na jeans hapo hachomoi kwenye mtindo huo.

Sambamba na hayo alizungumzia namna alivyoweza kupiga hatua na mafanikio aliyoyapata kutokana na kazi hiyo ikiwemo amethubutu kutoka nyumbani kuanza kujitegemea mwenyewe

Vile vile alisema kuna kuipato pia anakipata kutokana na kazi hiyo tofauti na hapo awali alivyokuwa hajaanza kufanya kazi yake.

“Nisiwe mnafiki na nisiseme uwongo kunakipato ambacho napata mpaka sasa japo sio kikubwa lakini Alhamdulillah tunasema wenyewe kidogo kuna mafanikio ambayo yanaoneka”alisema

Kitu gani kinakupa furaha kwenye maisha yako?

“kitu kinachonipa furaha kwenye maisha yangu nipale ninapoona kazi yangu watu wanaifurahia na nikiona carrier yangu inakua siku hadi siku nakumbuka nilianza na followers mmoja hadi sasa nina 55k”alisema.

Jackie8 alimaliza Mahenge primary school, na kuendelea na masomo ya  Sekondari  katika shuke ya Feruzi Samigo iliyopo kigamboni na baadaye akajiunga na Advance Loyola High school.

 Jackie8 anamiaka takribani mitatu kwenye kazi yake, ameanza kutoa video yake ya kwanza mwaka 2018.

Ebwana eeh!!! Nikwambie tu kila kitu ambacho unacho tambua kua huo ni mbadala wa elimu yako komaa na ujuzi, ubunifu au kipaji chako hakika utatoka tu have a nice Monday!!!!!.

 

 






Comments 1


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags