Katika ‘jezi’ hizo sita zitakuwepo ‘jezi’ mbalimbali alizotumia katika michuano hiyo ikiwemo alizovaa kipindi cha kwanza katika fainali, nusu fainali, robo na za mechi ya 16 bora dhidi ya Australia na nyingine mbili za michezo ya hatua ya makundi.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Messi ameeleza kuwa sehemu ya mapato kutokana na mnada huo utapelekwa katika hospitali ya watoto ya Sant Joan de Déu (SJD) iliyoko Barcelona ili kukidhi mahitaji ya watoto wanaougua magonjwa adimu.
Mnada huo unatarajiwa kufanywa katika mtandao wa Sotheby's kuanzia Novemba 30 - Desemba 14.
Leave a Reply