Jinsi ya kufanya tafiti ya kuvutia ukiwa chuoni

Jinsi ya kufanya tafiti ya kuvutia ukiwa chuoni

Na Michael Anderson

Nikizungumza kuhusiana na kufanya tafiti ‘research’ kwa wanafunzi wa chuo si jambo geni kabisa, mara nyingi hupewa wanafunzi wanaokaribia kuhitimu na wale wanaoingia mwaka wa tatu.

Wanafunzi wengi huwa wanafeli katika tafiti zako kutokana na baadhi yao kutochagua kitu chepesi na wanachokielewa huku wengine wakizima moto katika tafiti zao bila kujua kuwa kazi hiyo huenda ikawa ndiyo sababu ya kupata kazi hapo baadaye.

 Jinsi ya kumaliza tafiti kwa haraka

  1. Chagua topic ambayo ni nzuri na unaweza kuifanya

Kuchagua topic nzuri itakuwia urahisi kuwapata respondents na watakuwa huru kukupa ushirikiano , nenda kafanye tafiti yako katika sehemu ambazo utapewa vibali vya kuingia sehemu yoyote utakayohitaji kuifanyia tafiti.

 

Pia uwe mjanja kuchagua topic ambayo hata akimaliza chuo inaweza kukusaidia, kuna baadhi ya taasisi ukienda kuomba kazi akionesha eneo alilotafiti na aina ya utafiti aliofanya inaweza ikawa sababu ya waajiri kukupatia ajira bila hata kupepesa macho.

  1. Tenga muda sahihi wa kufanya tafiti yako

Baadhi ya wanafunzi wamekuwa wakikimbizana na muda siku hizi wanaita zima moto, so ili kumaliza tafiti yako kwa haraka zaidi ni vyema ukatumia muda uliopewa kuifanya tafiti hiyo kwani zima moto inaweza kupelekea tafiti yako isiwe bora huku baadhi ya vitu kukosekana.

  1. Omba msaada kwa wahitimu waliyopita

Waswahili wanasema hakuna kitu kipya kila kitu cha zamani so jitahidi katika tafiti yako kuzungumza na watu ambao wamehitimu, hii inaweza kukusaidia kupata materia na kukupa njia nzuri ya kukamilisha kwa mapema research yako.

Hayo machache yanaweza kuwa ndiyo ya muhimu kabisa ya kukusaidia wewe kumaliza tafiti yako kwa haraka zaidi lakini lipo jambo la muhimu ambalo litapelekea tafiti (research) yako kupendwa na kila mtu nalo ni ‘kuchagua title inayoeleweka’.

 Title ya research inatakiwa ibebe kile ulichokieleza katika utafiti wako na kiwe cha kuvutia ili kuteka akilia ya msomaji anapoanza kuipitia kazi yako basi title isimuache na maswali kuwa ulikuwa unamaanisha nini.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags