Ikiwa una tatizo la kusahau 'kusevu' namba za simu ulizopigiwa, kisha unapata shida kuzipata fuata njia hii ili kuzirudisha utakapozihitaji.
Ingia play store kisha pajua app iitwayo SMS Backup & Restore. App hii inapatikana katika simu ya Android, ukishapakua ifungue na kisha ubonyeze eneo lililoandikwa Get Started kisha katika permission mbalimbali
Bonyeza eneo lililoandikwa set up a backup, kisha bonyeza next iliyopo chini kulia. Baada ya hapo utafunguka ukurasa mwingine ambapo utachagua unapotaka kuhifadhi namba za simu ulizopigiwa, inaweza kuwa Google Drive , Dropbox au kwenye simu na ubonyeze tena next ambapo utatakiwa kuchagaua muda wa kuhifadhi simu ulizopigiwa.
Unaweza kuchagua mwezi , wiki au kila baada ya saa. Ukichagua muda bonyeza eneo lililoandikwa back up now lililopo chini upande wa kulia wa simu kwa kufanya hivyo utaweza kurudisha namba za simu ulizopigiwa.

Leave a Reply